'Hit em up' ya Tupac ndiyo nyimbo bora ya Muda ote ya Hi-hop Billboards
Sisti Herman
May 26, 2024
Share :
Wimbo wa marehemu Tupac Shakur uitwao ‘Hit Em Up’ umetajwa na Billboard kuwa ndiyo wimbo bora wa muda wote huku ukishika nafasi ya kwanza katika tovuti hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Billboard wimbo huo ulioachia mwaka 1996 kwa ajili ya kuwachana wasanii wenzake marehemu Biggie Smalls, Junior M.A.F.I.A., na Mobb Deep, ndio ngoma bora inayokimbiza zaidi katika orodha ya nyimbo 15 za Hip-hop.
Katika orodha hiyo ngoma tano ambazo zinakimbiza zaidi ya kwanza ikiwa ya Tupac, ‘The Story of Adidon’ ya Pusha T, ‘Supa Ugly’ ya Jay-Z, ‘No Vaseline’ ya Ice Cube na ‘Meet the Grahams’ kutoka kwa Kendrick Lamar.
Tupac Shakur alifariki Septemba 7, 1996, baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye gari huko Las Vegas, Nevada.