Hitilafu yasababisha wateja kujizolea mipesa ya bure Benki
Eric Buyanza
March 19, 2024
Share :
Benki ya kibiashara nchini Ethiopia inajaribu kurejesha mamilioni ya dola zilizochukuliwa na wateja kufuatia kile ilichokitaja kama hitilafu ya mifumo.
Zaidi ya dola milioni 40 ziliripotiwa kuotolewa kwenye Benki ya Biashara ya Ethiopia inayomilikiwa na serikali.
Hayo yalijiri baada ya wateja kugundua wanaweza kutoa pesa zaidi ya zile walizokuwa nazo kwenye akaunti zao.
Hali hiyo ilichukua masaa kadhaa kabla ya Benki kuamua kuzima mitambo na kusimamisha shughuli zake zote.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu inadaiwa ni kati ya watu waliojizolea pesa nyingi kutokana na hitilafu hiyo na tayari msako mkali umeanzishwa ili kuweza kuhakikisha kila aliyechukua pesa ambayo sio yake anarudisha.