pmbet

Hizi hapa sababu za Ancelotti kumwita Neymar kikosini

Eric Buyanza

May 20, 2026
Share :

Kocha wa Brazil Carlo Ancelotti amesema kuwa hali ya kimwili ya Neymar ‘imeboreka’, lakini atakuwa na ‘majukumu sawa’ na wachezaji wengine wa Brazil kwenye Kombe la Dunia.

 

Kocha huyo wa zamani wa Real Madrid amesema kwa msimu mzima wamekuwa wakitathmini utimamu wa Neymar na kuona ameimarika na kwa kuwa ni mchezaji muhimu wameona wamjumuishe kwenye kikosi kitakachoshiriki kombe la Dunia.

 

Ancelotti amesema Neymar atakuwa akitumika pale inapohitajika kutokana na uzeofu wake.

 

"Neymar atakuwa na majukumu sawa na wachezaji wengine 25, ana nafasi ya kucheza, au kutocheza, kukaa benchi au kutambulishwa kama mbadala"

"Ana jukumu sawa na wengine, yeye ni mchezaji mwenye uzoefu....katika baadhi ya majukumu kwenye goli na ushambuliaji tumetoa kipaumbele kwenye uzoefu" alisema Ancelotti.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet