pmbet

Hizi ndizo mbinu za kulinda figo zako

Eric Buyanza

December 15, 2023
Share :

1. PUNGUZA ULAJI WA CHUMVI: 
Chumvi nyingi katika lishe yako inaweza kuongeza shinikizo la damu na hatari ya ugonjwa wa figo. Kula vyakula vyenye chumvi kidogo kama matunda, mboga, na nafaka nzima.
 

2. KUNYWA MAJI YA KUTOSHA: 
Maji ni muhimu kwa figo zetu kufanya kazi vizuri. Kunywa angalau lita mbili za maji kwa siku ili kusaidia figo kuondoa taka na sumu kutoka kwenye mwili wako.
 

3. EPUKA KUNYWA POMBE KUPITA KIASI: 
Unywaji wa pombe kupita kiasi unaweza kuathiri vibaya figo zako.
 

4. FANYA MAZOEZI YA MARA KWA MARA: 
Mazoezi ya kimwili hupunguza hatari ya ugonjwa wa figo kwa kuongeza mtiririko wa damu na kudhibiti shinikizo la damu. Fanya angalau dakika 30 za mazoezi ya wastani kwa siku.
 

5 KULA LISHE BORA:
Lishe yenye afya inayoongozwa na matunda, mboga, protini nzuri na nafaka nzima inaweza kusaidia kulinda figo zako. Epuka vyakula vyenye mafuta mengi, sukari na vyakula vyenye chumvi nyingi.
 

6. DHIBITI VIZURI KIWANGO CHA SUKARI MWILINI: 
Ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa husababishwa na kisukari, hivyo ukizuia kisukari umefanikiwa kulinda figo yako. Nenda hospitali yoyote wakupime kiwango cha sukari na daktari akushauri nini cha kufanya angalau mara tatu kwa mwaka.
 

7. EPUKA SIGARA: 
Sigara inaweza kusababisha uharibifu wa figo na kuongeza hatari ya ugonjwa wa figo. Ni bora kuacha kabisa sigara ili kulinda figo zako.
 

8. PUNGUZA MATUMIZI YA DAWA ZA KUTULIZA MAUMIVU:
Dawa za kutuliza maumivu kama vile ibuprofen na paracetamol zinaweza kusababisha uharibifu wa figo ikiwa hutumiwa kwa muda mrefu au kwa kipimo kikubwa. Tumia dawa hizi kwa kuzingatia maelekezo ya daktari.
 

9. TAFUTA MATIBABU MAPEMA: 
Ikiwa una dalili yoyote ya matatizo ya figo kama vile mkojo mweusi, uvimbe, au maumivu ya mgongo, tafuta matibabu haraka. Kuchelewesha matibabu kunaweza kusababisha madhara zaidi kwa figo zako.
 

11. PIMA AFYA YA FIGO ZAKO WALAU MARA MOJA KWA MWAKA: 
Tembelea hospitali yoyote yenye vifaa utapatiwa huduma, hii itakusaidia kujua afya ya figo zako.
 

12. DHIBITI UZITO WAKO:
Uzito husababisha figo kulemewa, uzito stahiki hujulikana baada ya kuoanisha uzito ulionao na urefu wako. Tembelea hospitali ujue uzito wako kama umezidi au umepungua sana uchukue hatua kupunguza au kuongeza calories. Watu wanene wanasumbuliwa na matatizo yote kama figo,moyo na n.k
 

13. ACHANA NA ULAJI WA VYAKULA VYA CHAPCHAP KAMA CHIPS: 
Ulaji vyakula vya haraka vyenye mafuta mengi kwa mfano chips, umetajwa kuwa hatari kwa afya ya binadamu, kwani husababisha maradhi mengi yasiyo ya kuambukiza hasa figo, moyo, shinikizo la damu kisukari na saratani za aina zote. Imeelezwa kuwa sahani moja ya chips kavu huwa na mafuta yanayokaribia nusu kikombe cha chai ambayo ni sawa na ujazo wa milimita 250.
 

14. DHIBITI SHINIKIZO LA DAMU: 
Shinikizo la damu linaweza kusababisha uharibifu wa figo. Chukua hatua za kudhibiti shinikizo la damu kama vile kula lishe yenye afya, kufanya mazoezi na kuepuka mkazo.
 

#Afya
AfyaYaFigo
#LindaFigo
#Pmtvtz
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet