Hospitali binafsi zasitisha kupokea wagonjwa wanaotumia kadi za NHIF
Eric Buyanza
February 29, 2024
Share :
Chama cha Watoa Huduma Binafsi wa Afya (APFTHA) kiazimia kuacha kupokea wagonjwa wenye kadi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuanzia leo.
Mwenyekiti wa chama cha hicho, Dk. Egina Makwabe amesema maazimio hayo yamefikiwa baada ya kikao kilichofanyika muda mfupi uliopita Jijini Dar es Salaam.
"Kuanzia saa sita usiku leo Alhamis Februari 29, hospitali binafsi tumeazimia hatutapokea mgonjwa mpya mwenye kadi ya NHIF na walioko wodini wenye hali mbaya (ICU) tutaendelea kuwahudumia ndani ya saa 48,".
Hospitali ambazo hazitapokea wagonjwa ni hizi zifuatazo;
Regency Hospital, Kairuki Hospital, Apolo Hospital pamoja na Hospitali zote za Aga Khan.