pmbet

Hospitali marufuku kuzuia wagonjwa au miili kwa sababu ya deni

Eric Buyanza

November 13, 2026
Share :

Wasimamizi wa hospitali za umma na binafsi nchini Kenya watatozwa faini ya hadi Shilingi milioni 2 (takriban Shilingi milioni 40.8 za Kitanzania) kwa kuwazuia wagonjwa wanaopaswa kuruhusiwa kuondoka au miili ya marehemu kwa sababu ya madeni ya matibabu.

 

Hatua hiyo imependekezwa katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya Afya wa 2024, ambao umepitishwa kwa kauli moja na wabunge na sasa unasubiri kutiwa saini na Rais William Ruto ili kuwa sheria.

Mswada huo unamulika hospitali zinazokataa kumhudumia mgonjwa au kumzuia kuondoka kwa sababu hajalipa bili au ameshindwa kulipa malipo ya awali ya matibabu. Pia mswada huo unakataza hospitali kuzuia miili ili kulazimisha familia kulipa gharama za matibabu.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Bunge, James Nyikal, alisema sheria hiyo itasaidia familia maskini ambazo zimekuwa zikiteseka baada ya wapendwa wao kuzuiliwa hospitalini kutokana na madeni.

 

Hata hivyo, mswada huo unaruhusu hospitali kuwataka wagonjwa au jamaa zao kutia saini hati ya ahadi ya kulipa deni.
Hati hiyo itaeleza muda na utaratibu wa kulipa deni na itakuwa na nguvu ya kisheria, hivyo hospitali zinaweza kuishtaki familia isipotimiza ahadi.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet