Huenda pauni milioni 40 zikampeleka Liam Delap Old Trafford
Eric Buyanza
April 2, 2025
Share :
Manchester United wanapambana kuhakikisha wanaipata huduma mshambuliaji wa Ipswich Town, Liam Delap huku majadiliano yakiripotiwa kuanza.
Kazi ya kuipata huduma ya Liam mwenye umri wa miaka 22 haitakuwa nyepesi kwa Manchester United kwa kuwa anawindwa pia na vilabu vya Liverpool, Chelsea na Newcastle.
Kipengele cha mkataba wa Delap kinaruhusu vilabu kumsajili kwa pauni milioni 40 ikiwa Ipswich ambao kwa sasa wana alama 12 watashuka daraja msimu huu.