pmbet

Huyu hapa kiumbe mwenye sura mbaya zaidi duniani

Eric Buyanza

August 6, 2026
Share :

Kiumbe anayetambulika rasmi kuwa na sura mbaya zaidi duniani ni samaki anayeitwa Blobfish. Samaki huyu alipigiwa kura na kutangazwa na taasisi ya Ugly Animal Preservation Society kuwa ndiye kiumbe hai mwenye sura mbaya kuliko wote duniani
 

Blobfish hana misuli thabiti wala mifupa migumu. Mwili wake una muundo wa jeli yenye msongamano mdogo kuliko maji.

 

Anapokuwa chini kabisa ya bahari shinikizo kubwa la maji linamfanya aonekane wa kawaida, ila anapovuliwa na kutolewa nje ndipo mwili wake unapochanika na kulegea, na kumfanya aonekane kama donge la jeli lenye pua kubwa na sura ya kusikitisha au kununa.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet