Huyu hapa Sugar, njiwa mzee zaidi duniani ameishi miaka 44
Eric Buyanza
May 14, 2026
Share :

Sugar, njiwa mweupe wa kufuga kutoka Chesterfield, Missouri nchini Marekani, aliyezaliwa tarehe 23 Juni mwaka 1981 ametambuliwa na Guinness World Records kama njiwa mzee zaidi duniani akiwa na umri wa miaka 44.
Njiwa wana wastani wa kuishi kwa karibu miaka 20, lakini njiwa huyu ameishi zaidi ya mara mbili ya muda huo.
Sugar ametumia muda mwingi wa maisha yake akiwa karibu na tajiri yake Dewayne Orender mwenye umri wa miaka 77, mara nyingi wakitazama TV na kusikiliza muziki.
Dewayne Orender alikuwa na matumaini kwamba njiwa wake angefikisha umri wa miaka 50, ili aweze kumfanyia tafrija kubwa, lakini cha kusikitisha Sugar alifariki Jumapili ya Pasaka ya mwaka huu.
Kabla ya rekodi ya sasa, njiwa maarufu wa kijeshi wa Ujerumani aliyeitwa Kaiser, aliyetekwa na jeshi la Marekani wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia, aliishi miaka 32 yaani 1917–1949.





