Huyu ndiye mwanamke tajiri kuliko wote duniani
Eric Buyanza
January 20, 2024
Share :
Anaitwa Françoise Bettencourt-Meyers, ana utajiri wa dola bilioni 100 za kimarekani na pia ni mtu wa 15 tajiri zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes.
FRANÇOISE NI NANI?
Ni mama mfanyabiashara na bilionea wa kifaransa mrithi wa kampuni ya vipodozi ya L'Oréal ambayo anamiliki 33% ya kampuni hiyo ya kifamilia.
Kwa sasa ana umri wa miaka 70 na alirithi utajiri huo kutoka kwa mama yake Liliane Bettencourt, aliyefariki dunia mwezi Septemba mwaka 2017 akiwa na miaka 94.
Babu yake Eugène Schueller ndiye aliyekuwa mwanzilishi wa kampuni ya L'Oréal.