Huyu sasa ni mdaka mikuki Aboubacar Khomeiny ni mali ya Yanga.
Joyce Shedrack
July 8, 2024
Share :
Klabu ya Yanga imethibitisha kukamilisha uhamisho wa golikipa Khomeiny Aboubacar kutoka Singida Black Stars kuwa golikipa wao mpya kuelekea msimu ujao.
Nyota huyo wa zamani wa Geita Gold anaongeza nguvu kwenye timu ya wananchi katika eneo la golikipa akitarajia kushirikiana na Djigui Diarra pamoja na Aboutwalib Mshery waliokuwepo kikosini hapo tangu msimu uliopita.