Ibenge kwenye majukumu mapya ya kumfundisha Diarra.
Joyce Shedrack
June 17, 2024
Share :
Kocha Mkuu wa zamani wa timu ya Taifa ya DRC, Rs Berkane na As Vita Jean Florent Ibenge huwenda akatimkia kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Mali kuchukua nafasi ya Éric Chelle ambaye alifukuzwa kazi hivi karibuni.
Ibenge ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Al Hilal SC ya Sudan,ni miongoni mwa makocha wanaotelewa macho kuchukua nafasi hiyo kutokana na mafanikio aliyoyapata kwenye michuano ya Kimataifa barani Afrika.
Kocha huyo aliwahi kuchukua kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2021/2022 akiwa na kikosi cha Rs Berkane ya Morocco, huwenda akawa kocha mkuu wa golikipa wa Yanga Djigui Diarra ambaye ni kipa namba moja wa timu ya Taifa ya Mali.
Ikumbukwe kuwa bado Ibenge ana mkataba na klabu ya Al Hilal hivyo ili Mali wafanikiwe kupata huduma yake itawalazimu kulipa hela ya kuuvunja mkataba huo.