Ibenge wa Azam FC atajwa timu ya Taifa Angola
Sisti Herman
February 16, 2026
Share :

Shirikisho la Soka la Angola (FAF) limeripotiwa kuwa kwenye hatua za mazungumzo ya kumteua Florent Ibenge (64) kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Angola, kuchukua nafasi ya Patrice Beaumelle (47), kocha wa Ufaransa ambaye hivi karibuni aliachana na shirikisho hilo kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Mazungumzo yanaendelea vizuri, wakati majadiliano yalilenga zaidi masharti ya kibinafsi ikiwa ni pamoja na mshahara ili kupata saini ya Ibenge ambaye ametoka kuifikisha Azam Fc hatua ya makundi ya michuano ya CAF.





