pmbet

Ibrahim Class atua Bungeni na Mikanda yake miwili ya WBC.

Joyce Shedrack

May 4, 2026
Share :

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahimu Mgenda, maarufu kama “Class”, leo ametinga ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma akiwa na mikanda yake miwili ya Ubingwa wa WBC.



Ibrahimu alifika Bungeni kufuatia mwaliko maalum wakati wa uwasilishwaji wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 chini ya Waziri Paul Makonda.

Ikumbukwe kuwa mnamo April 25 mwaka huu, @ibrahimuclass aliweka rekodi ya kipekee nchini na barani Afrika baada ya kutwaa mikanda ya WBC International Silver Belt na WBC International Gold Belt (uzito wa Super Featherweight), kwa kumchakaza Kritiphak Duangnut wa Thailand kwa TKO raundi ya 5.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet