pmbet

Idadi ya waliofariki kwa tetemeko Japan yazidi kuongezeka

Eric Buyanza

January 2, 2024
Share :

Idadi ya watu waliofariki katika tetemeko kubwa la ardhi nchini Japan lililosababisha nyumba kubomoka na mabarabara kukatika sasa wamefikia 30.
 

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani, vifo vyote vimetokea katika mkoa wa Ishikawa, kwenye pwani ya kaskazini-magharibi ya Japan, ambapo kilikuwa kitovu cha tetemeko hilo la Jumatatu.
 

Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida amesema takribani wanajeshi 1,000 wako katika juhudi za uokoaji kwenye maeneo yaliyokumbwa na tetemeko.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet