pmbet

Idobale, salamu ya heshima inayosalimiwa na wanaume tu!

Eric Buyanza

July 23, 2026
Share :

Idobale ni salamu ya heshima na unyenyekevu mkubwa katika utamaduni wa Wayoruba kutoka magharibi mwa Nigeria inayofanywa na wanaume pekee.

 

Mwanaume hulala kabisa chini, kifua na tumbo vikigusa ardhi, huku mikono yake ikiwa imeelekezwa mbele au pembeni mwa mwili wake.

 

Salamu hii hutumika sana unapomsalimia mzazi, mzee yeyote katika jamii, au chifu/mfalme. Pia ni sehemu ya lazima kwenye posa na harusi za kitamaduni, ambapo bwana harusi na marafiki zake hulala chini mbele ya wazazi wa bibi harusi kuomba ridhaa ya ndoa na baraka.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet