Idris Sultan kuipeperusha bendera ya Tanzania uso kwa uso na Rais wa Nigeria.
Joyce Shedrack
July 25, 2024
Share :
Msanii wa filamu za Bongo Idris Sultan anatarijia kukutana uso kwa uso na Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu akiipeperusha bendera ya Tanzania kwenye moja ya Tamasha kubwa Afrika Nchini Nigeria linalojulikana kama Global Enterneurship Festival.
Idris Sultan ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram akitangaza kuwa amechaguliwa kuwa balozi wa Tamasha hilo kubwa Afrika la Global Enterneurship Festival, litakalohudhuriwa na watu zaidi ya 3000 kutoka mataifa zaidi ya 67 ulimwenguni mwezi Novemba mwaka huu.
Msanii huyo ambaye ni muigizaji na mchekeshaji mkubwa Tanzania atakuwepo nchini Nigeria kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwaka huu kwa ajili ya kuhudhuria tamasha hilo.