'IFUNANYA' - Jennifer Lopez apata jina la Kinigeria!
Eric Buyanza
February 19, 2024
Share :
Muigizaji na mwanamuziki wa Marekani, Jennifer Lopez, amejibatiza jina 'IFUNANYA' kama jina lake la Ki-Nigeria.
Jeniffer alikuwa kwenye mahojiano na mwanahabari maarufu wa Nigeria, Drea Okeke na ndiye aliyependekeza jina hilo kwa Lopez wakati wa mahojiano hivi karibuni.
Ifunanya inamaanisha 'Upendo' katika lugha ya kabila la Kiigbo la nchini humo.
Akiwa kwenye mahojiano Lopez aliuliza "Jina langu [la Nigeria] ni nani?"
Okeke akajibu: "Ni Ifunanya...jina hilo linamaanisha 'Upendo'. . Hilo ndilo jina lako mpenzi"
Lopez: "Ifunanya! Niite Ifunanya" akasema Lopez akionesha kulifurahia jina hilo.
Mwanahabari huyo pia alimpa jina mume wa Lopez, Ben Affleck, na kusema jina lake litakuwa 'Obim' ikiwa na maana ya 'moyo wangu'.