Ihefu wasitisha mkataba na C.E.O
Sisti Herman
January 4, 2024
Share :
Uongozi wa timu ya Ihefu Sc ya ligi kuu Tanzania umetoa taarifa kwa umma ya kufikia makubaliano ya pande mbili ya kusitisha Mkataba wa kazi na aliekua Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Ndugu. Biko Mangasini Scanda ambaye alitambulishwa kwenye nafasi hiyo wikichache zilizopita.
Pia Biko kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii ametoa waraka wa kuiaga timu hiyo ulosomeka;
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Ihefu kwa kunipa Nafasi ya Kuwa mtendaji mkuu lakini pia naishukuru kwa kunipa nafasi tena ya Kuendelea na changamoto mpya za kuutumikia Mpira wa Tanzania.
Napenda kuwashukuru Wapenda Soka wote kwa kuniunga Mkono kwa namna moja ama nyingine na pia ndoto kubwa ya maono yetu vijana wa Tanzania bado inaendelea na hivyo tunatakiwa kuendelea na mchakato wa Kuusaidia mpira wa nchi hii.
Mwisho kipekee Kabisa nimshukuru Fahad Pirmohamed mmiliki wa Ihefu kwa moyo wake na Utu, niwashukuru wachezaji wote kwa heshima kubwa walonipa na namna wameapa kuipigania Chapa ya IHEFU. Hakika Familia yetu ilikua na Furaha pamoja.
Ulitamatika hivyo waraka wa Biko.