Ihefu yabadiishwa jina kuwa Singida Black Stars
Sisti Herman
April 3, 2024
Share :
Uongozi wa Ihefu FC umeyahamisha makazi ya klabu hiyo kutoka Mbarali Mbeya na kwenda mkoani Singida, na hivyo kufanya mabadiliko ya jina la timu na sasa kutambulika kama Singida Black Stars Sports Club.
Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imesema lengo la kubadilisha jina la timu ni kuiunganisha na wananchi wa mkoa wa Singida.
Pia taarifa imeeleza kuwa taratibu zote za usajili wa jina hilo tayari zimekamilika kwa kufuata miongozo, kanuni na taratibu zote za Nchi, Baraza la Michezo (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).