Ijue safari fupi zaidi ya ndege duniani, inatumia Dakika 2
Eric Buyanza
June 27, 2024
Share :
Safari ya ndege huko Scotland, kati ya visiwa vya Westray na Papa Westray inashikilia rekodi ya dunia ya kuwa safari fupi zaidi kwa kutumia ndege duniani.
Safari hiyo ni ya kilomita 2.74 na huchukua dakika mbili tu au wakati mwingine chini ya hapo kutegemeana na hali ya hewa.
Britten-Norman Islander ndiyo ndege ndogo yenye yenye uwezo wa kupakia abiria 8 na rubani mmoja, na ndiyo imekuwa ikitumika kusafirisha abiria tangu mwaka 1967.
Bei ya tiketi ya safari hiyo kutoka kisiwa kimoja kwenda kingine ni Dollar 22 (sawa na shilingi 57,000 za kibongo)
Watu wanaokaa kwenye visiwa hivyo wana machaguo mawili tu, la kwanza ni kupanda pantoni inayopita kwenye bahari yenye vimbunga vikali au kupanda ndege hiyo ambayo ndio imekuwa chaguo la watu wengi.