pmbet

Ikitokea tumeshindwa kufuzu robo fainali, tutakuwa tumerudi kwenye malengo yetu - Ali Kamwe

Eric Buyanza

December 9, 2023
Share :

TUKISHINDWA KWENDA ROBO, ITAKUA FUNZO - ALI KAMWE

Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amefunguka mara baada ya sare ya 1-1 ugenini kwa Medeama kwenye mchezo wa raundi ya 3 ya ligi ya mabingwa Afrika kwenye kundi D.
 

"Hesabu tulizopanga zinakwenda vizuri mpaka sasa, tulitamani kushinda katika michezo mitatu ya kwanza, lakini kwasababu kuna mzunguko wa pili, kuna alama zingine 9 za kupambana" alisema Kamwe.
 

"Hatukucheza hatua ya makundi kwa miaka 25, lakini tumefika leo, hatutaki kusema bado hatuna fursa ya kwenda robo fainali, nafasi bado ipo na Yanga itapambana hadi jasho la mwisho ili kuhakikisha tunakwenda robo fainali" aliongeza Kamwe.
 

"Ikitokea tumeshindwa kufuzu robo fainali, tutakuwa tumerudi kwenye malengo yetu mama, kufika makundi, tumejifunza kwenye hatua ya makundi ili wakati mwingine tukitaka kwenda robo fainali nini unapaswa kufanya" alimaliza Kamwe

Yanga bado inaendelea kuburuza mkia wa kundi D ikiwa na alama 2 kwenye mechi 3 kwenye kundi lenye timu kama Al Ahly, CR Belouizdad na Medema.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet