Ikiwa Hamas hawatasalimisha silaha tutawapokonya - Trump
Eric Buyanza
October 16, 2025
Share :
Rais wa Marekani Donald Trump amesema "itawapokonya silaha" Hamas ikiwa hawatoweka chini silaha.
"Ikiwa hawatasalimisha silaha zao wenyewe, tutawapokonya," alisema Rais huyo wa Marekani akiwa Ikulu ya White House mbele ya waandishi wa habari.
Hata hivyo Trump hakuweka wazi wala kutoa maelezo juu ya namna operesheni hiyo ya upokonyaji silaha itakavyofanyika.