pmbet

Ikulu yathibitisha Trump kuwepo kwenye fainali ya Kombe la Dunia.

Joyce Shedrack

July 17, 2026
Share :

Ikulu ya Marekani (White House) imethibitisha kuwa Rais Donald Trump atahudhuria mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia utakaochezwa Jumapili kati ya Uhispania na Argentina.

Donald Trump: US president 'will move World Cup games from unsafe cities' -  BBC Sport

Huu utakuwa mchezo wa kwanza ambao Trump atahudhuria katika mashindano hayo, licha ya kuonyesha mara kadhaa kuunga mkono mchezo wa soka na kushiriki katika maandalizi ya mashindano hayo.

 

Rais wa FIFA Gianni Infantino, tayari amethibitisha kuwa Trump atashiriki katika hafla ya kukabidhi kombe kwa timu itakayotwaa ubingwa baada ya mchezo huo kumalizika.

 

Mwaka uliopita Trump aliikabidhi Chelsea FC kombe la Dunia la klabu huku akijenga uhusiano wa karibu na Infantino. Hata hivyo, hivi karibuni alizua mjadala baada ya kukiri kuwa aliwasiliana na FIFA kuhusu kadi nyekundu aliyopewa Folarin Balogun ambayo baadaye ilisimamishwa.

 

Fainali hiyo inatarajiwa kuvuta hisia za mamilioni ya mashabiki duniani huku uwepo wa Rais Trump ukiongeza uzito na mvuto wa tukio hilo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet