pmbet

Ili mwanamke apate ajira ya polisi nchini Indonesia, lazima awe mrembo na bikira

Eric Buyanza

May 25, 2024
Share :

Huko nchini Indonesia, inaelezwa kuwa wanawake wanaotaka kuwa maafisa wa polisi moja ya masharti ni lazima uwe 'mrembo' na pia 'Bikira'.

Japo jambo hilo halisemwi rasmi, lakini wanawake waliowahi kuhitaji ajira hiyo wanaripoti kuwa walifanyiwa vipimo vya ubikira kama sehemu ya mchakato wa ajira.

Andreas Harsono kutoka Human Rights Watch anasema polisi wa Indonesia wanaamini jamii haitamkubali afisa wa polisi wa kike ambaye ameshawahi kujihusiha na ngono.

Mwanamke aitwae Zakia na ambaye jina lake la mwisho halikutajwa ili kulinda utambulisho wake aliiambia Human Rights Watch katika malalamiko yake kwamba alifeli mtihani wake alipoomba kazi hiyo baada ya kufanyiwa kipimo cha 'ubikira'.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet