pmbet

IMETOSHA! Reiss Nelson aondoka Arsenal baada ya miaka 18

Eric Buyanza

August 28, 2026
Share :

Klabu ya Arsenal imetangaza rasmi kusitisha mkataba wa winga wake wa pembeni, Reiss Nelson, kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Uamuzi huu unamfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuwa mchezaji huru (free agent), huku klabu mbalimbali za Ligi Kuu ya Uingereza na barani Ulaya zikianza mbio za kuwania saini yake kabla ya dirisha la usajili kufungwa.


Chini ya kocha Mikel Arteta, Nelson alishindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Historia yake ya kukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara ilishusha kiwango chake na kumfanya akose muendelezo mzuri wa fomu yake ya soka.

 

Mchezaji huyo alikuwa akipokea mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki. Kuondoka kwake kunaipa Arsenal unafuu mkubwa wa kifedha kwenye bajeti ya mishahara.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet