"Inahuzunisha sana", Redknapp asikitishwa na kiwango cha Rashford!
Eric Buyanza
April 1, 2024
Share :
Kiungo wa zamani wa Liverpool Jamie Redknapp amesema anajisikia 'huzuni kubwa' anapotazama mapambano anayopitia Marcus Rashford kipindi hiki pale Old Traford.
Rashford mwenye umri wa miaka 26 amepata ugumu kuonyesha kiwango chake klabuni hapo akiwa amefunga mabao 8 pekee na asisti 6 katika mechi 36 katika mashindano yote aliyocheza.
Mshambuliaji huyo amekuwa na wakati mgumu muhula huu, na kumekuwa na tetesi kwamba yuko katika hatari ya kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha England kitakachoshiriki Euro 2024.
MANENO YA REDKNAPP
"Marcus Rashford ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu..."Mungu amempa kila kitu...ana umbile zuri, anaweza kukimbia, anapiga chenga, anaweza kupiga mashuti na alifunga mabao 30 mwaka jana”.
"Nikimtazama sasa. Nadhani ana mabao 8, 7 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza na moja kwenye Kombe la FA....Anaonekana hafurahii kabisa soka lake. Na kwangu jambo hili linanisikitisha sana." Redknapp aliiambia Sky Sports.