Inaki aiwahi Barca baada ya Ghana kutoka Afcon
Sisti Herman
January 24, 2024
Share :
Iilikuwa swala la muda tu Ghana kutoka kwenye michuano ya Afcon 2023 kwenye hatua ya makundi kwani mazingira ya nje ya uwanja hayakuonyesha utayari wa wachezaji wao wengi kushiriki kwa muda mrefu mashindano hayo akiwemo Inaki Williams wa Athlethic Bilbao ya ligi kuu nchini Hispani.
Akili za wachezaji wengi wa Ghana hazikuwa kwenye mashindano hayo, hiyo inadhihirika wazi baada ya mchezo wa makundi ambao umetamatika jana jioni kwa sare ya 2-2 dhidi Msumbiji na timu hiyo kushindwa kufuzu hatua ya mtoano, mshambuliaji huyo mzaliwa wa Hispania aliwahi haraka kwenye ndege binafsi aliyokuja nayo kurejea Hispania.
Inaki amerejea Hispania ili kuwahi mchezo wa ligi wa La Liga dhidi ya Barcelona leo usiku, kimwili walikuwa AFCON ila kiakili walikuwa Ulaya.