INATISHA: Polisi arekodiwa akimkanyaga mtu kichwani uwanja wa ndege
Eric Buyanza
July 25, 2024
Share :
Huko nchini Uingereza Afisa wa polisi amerekodiwa akimpiga mtu huku akimkanyaga kichwani, tukio ambalo limetokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Manchester.
Mwanaume anayepigwa anaonekana kwenye video iliyosambaa mitandaoni akiwa amelala kifudifudi, huku askari huyo akiendelea kumpiga.
Hasira za wananchi kuhusu unyanyasaji huo imekuwa kubwa na mamia ya watu waliandamana nje ya kituo cha polisi huko Rochdale, Greater Manchester siku ya Jumatano kulaani kitendo hicho. Angalia video hapo chini