pmbet

INATISHA: Wakubali kunyanyaswa kingono ili wapate chakula

Eric Buyanza

July 22, 2024
Share :

Wanawake kadhaa waliokimbia mji wa Omdurman nchini Sudan wamesema kuwa kufanya mapenzi na wanajeshi ndiyo njia pekee inayowawezesha kupata chakula au bidhaa ambazo wataweza kuuza ili kupata pesa za kulisha familia zao, limeripoti gazeti la Guardian la nchini Uingereza.

Muathiriwa mmoja alisema matukio hayo hufanyika katika baadhi ya viwanda ambako chakula cha akiba ya nchi kimehifadhiwa.

"Wazazi wangu wote wawili ni wazee na wagonjwa na sijawahi kumruhusu binti yangu kwenda kutafuta chakula. Nilienda kwa askari na hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kupata chakula - walikuwa kila mahali katika eneo la viwanda," alisema mwanamke, ambaye alilazimishwa kufanya mapenzi na askari katika kiwanda cha kusindika nyama.

Matukio hayo yameripotiwa kuanza mara baada ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet