pmbet

INATISHA: Watoto wagundua mafuvu 17 wakati wakitafuta kuni

Eric Buyanza

July 31, 2024
Share :

Mafuvu 17 ya binadamu yaliyohifadhiwa kwenye masanduku ya chuma yamegunduliwa siku ya Jumatatu nchini Uganda kwenye eneo ambalo linashukiwa kuwa la kufanyia ibada.

Watoto waliokuwa wakitafuta kuni ndio waliogundua mafuvu hayo kwenye kijiji cha Kabanga karibu na mji wa Mpigi, magharibi mwa mji mkuu wa Kampala.

"Tulifanya uchimbaji kwenye eneo hilo, na tukapata mafuvu 17 ya vichwa vya watu," alisema msemaji wa polisi wa eneo hilo Majid Karim.

“Tunafanya uchimbaji zaidi ili kuhakikisha hakuna mafuvu zaidi ya yale tuliyoyapata hadi sasa,” amesema na kuongeza kuwa mabaki hayo yanachunguzwa ili kubaini umri na jinsia, pamoja na tarehe ambayo watu hao walizikwa. Polisi itafungua uchunguzi kubaini ni nani "anaweza kuwa alihusika na kitendo hiki", amesema Majid Karim. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet