pmbet

INATISHA: Watu 49 wafariki kwa kiu nchini Niger

Eric Buyanza

June 6, 2026
Share :

Tukio baya limetokea jangwani kaskazini mwa Niger. Makumi ya raia wa Niger wamefariki kwa kiu baada ya lori lililokuwa likiwasafirisha kutoka nchi jirani ya Mali kuharibika. Gavana wa Agadez ametangaza tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii siku ya Alhamisi hii, Juni 4. Thadhari ilitolewa na abiria wawili, ambao walifanikiwa kufika mji wa Assamaka baada ya kutembea kilomita kadhaa.

 

Picha za miili hiyo ikiwa jangwani, chini ya jua kali, ziliambatana na chapisho kutoka kwa gavana wa Agadez siku ya Alhamisi, Juni 4. Watu arobaini na tisa walifariki kwa kiu katika eneo hili la Niger linalopakana na Mali na Algeria. Raia hawa wa Niger waliondoka Harouba, katika nchi jirani ya Mali, mji unaojulikana kwa maeneo yake ya uchimbaji dhahabu, kusherehekea Eid na familia zao.

 

Lakini lori lililokuwa likiwasafirisha linaripotiwa kupotea kabla ya kuharibika baada ya siku kadhaa barabarani jangwani. Abiria "walikwama katikati ya mazingira magumu," yaliyojaa na halijoto kali na ukosefu wa vifaa.
 

Tahadhari ilitolewa na abiria kadhaa. Abiria wawili walifanikiwa kufika mji wa Assamaka baada ya kutembea kilomita kadhaa. Mamlaka za eneo hilo kisha zilituma ujumbe kwenda eneo la tukio na kugundua mkasa huo. Watu 49 waliopatikana wamekufa walizikwa katika eneo hilo la tukio.

 

Wakati wa safari yao ya kurudi, ujumbe huo ulikutana na gari lingine ambalo lilikuwa limekwama kwa siku tatu. Wakati huu, abiria 60 waliokolewa. Matukio haya, gavana aliandika, yanatumika kama ukumbusho wa “gharama ya kibinadamu ya kusafiri kupitia mojawapo ya mazingira magumu zaidi duniani.”
 

Eneo hilo, ambalo pia ni kituo cha usafiri kinachotumiwa na wahamiaji wanaojaribu kufika Ulaya, mara kwa mara huwa eneo la majanga ya aina hii.
 

RFI

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet