pmbet

Inatoka mashine inaingia mashine Olmo kumrithi De Bruyne.

Joyce Shedrack

July 17, 2024
Share :

Mabingwa wa Ligui Kuu ya Uingereza Manchester City ipo kwenye hatua za mwisho kumalizana na  klabu ya RB Leipzig ili kunasa saini ya mchezaji wao raia wa Uhispania Dani Olmo kwa dau la €51m.

 

Man City inahitaji huduma ya Nyota huyo wa Timu ya Taifa ya Uhispania ili kuziba pengo la kiungo wao Kevin De Bruyne anayetajwa kutimkia Saudi Arabia.

 

Olmo msimu uliopita kwenye ligi kuu ya Ujerumani amefunga magoli 8 na kutoa pasi za mwisho za magoli 5 katika michezo 25 huku kwenye michuano ya Mataifa ya Ulaya Euro 2024 akishinda tuzo ya mfungaji bora baada ya kufunga magoli matatu na kutoa pasi 2 za magoli.

Kiungo huyo huwenda hivi karibuni atawasili rasmi katika Jiji la Manchester kwa ajili ya kufanyiwa vipimo pamoja na kusaini nyaraka zote za kukamilisha uhamisho wake na kutambulishwa rasmi kama mchezaji timu hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet