India leo yazindua Treni inayopita chini ya maji
Eric Buyanza
March 6, 2024
Share :
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi leo Jumatano amezindua treni ya kwanza nchini humo inayopita chini ya maji kutoka mji wa Kolkata kwenda Howrah.
Modi alizindua kwa kufanya safari ya kwanza chini ya maji akiwa kwenye treni hiyo ambayo imekuwa gumzo akiwa amejumuika na wanafunzi.
Baadaye alipost picha kadhaa kwenye akaunti yake rasmi ya X (zamani Twitter), akisema: "Ziara ya Metro imeacha kumbukumbu ya kudumu kwa wote waliohusika katika mradi huo...tumepita kwenye handaki chini ya Mto Hooghly.”