Ingewezekana ningejipigia kura kushinda Ballon d'or 2026!
Eric Buyanza
September 8, 2026
Share :

Mshambuliaji nyota wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappé, amezua mjadala mzito kwenye ulimwengu wa soka baada ya kutangaza wazi kuwa angejipigia kura mwenyewe kama angekuwa mmoja wa wajumbe wanaochagua mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or 2026.
Katika mahojiano ya kipekee na majarida ya L'Équipe na France Football, Mbappé alionyesha kujiamini mnoo kuelekea sherehe za utoaji wa tuzo hizo zitakazofanyika jijini LondonOktoba 26, 2026.
Licha ya ushindani mkali kutoka kwa mastaa wengine waliofanya vizuri msimu huu, staa huyo mwenye umri wa miaka 27 hajaonyesha hofu yoyote.
“Ningejipigia kura mimi mwenyewe kushinda Ballon d'Or... Ninaamini kabisa kwamba ninaweza kuishinda mwaka huu, kwa hiyo sijaiondoa akili yangu kwenye hili,” alikaririwa Mbappé katika mahojiano hayo.
Mshambuliaji huyo alitetea msimamo wake kwa kueleza kuwa tuzo ya Ballon d'Or imekusudiwa kutathmini uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ndani ya uwanja, na si mafanikio ya timu pekee.
“Hii ni tuzo ya mtu binafsi, na kile ambacho mchezaji amekionyesha kwa kiwango cha mmoja mmoja ndicho kinachozingatiwa,” aliongeza Mbappé.





