Inonga aaga Simba
Sisti Herman
June 24, 2024
Share :
Beki wa klabu ya Simba raia wa Congo DR, Henock Inonga Baka kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram amewaaga mashabiki wa klabu hiyo.
"Asanteni sasna familia nzima ya Simba (akiweka imoji za Simba) nipo hapa kusema asante kwa yote mliyonifanyia na leo nasema kwaherini. kwaherini mtaendelea kubaki kwenye moyo wangu" aliandika Inonga kupitia chapisho hilo ambalo hata hivyo amelifuta kwenye mtandao wake wa kijamii.
Inonga anahusishwa kujiunga na AS FAR ya ligi kuu nchini Morocco.