pmbet

Inonga arudi kuwavaa Asec

Sisti Herman

February 18, 2024
Share :

Mara baada ya kuisha kwa michuano ya AFCON 2023 kutamatika wiki iliyopita na timu yake ya Taifa ya Congo DR kufanikiwa kufika nusu fainali, beki tegemeo wa klabu ya Simba Henock Inonga amejiunga rasmi kwenye kambi za mazoezi ya klabu hiyo inayojiandaa na mchezo wa raundi ya 5 ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Asec Mimosas baada ya mapumziko ya siku chache tu.

 

Simba inajiandaa kuwavaa Asec ikiwa inamtegemea beki huyo kwani tangu kuondoka kwake beki mwenza, Che Malone Fondoh amekuwa akibadilishiwa watu tofauti wakucheza nao kwenye nafasi hiyo hali iliyotafsiriwa kuwa ni kukosekana kwa mtu sahihi wa kuziba pengo la Inonga lililokuwa wazi tangu aondoke.

 

Simba itasafiri mapema wiki ijayo kuwafuata Asec Mimosas, mchezo utakaochezwa dimba la Alasabe Outarra huko Ivory Coast.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet