Inter Miami yampongeza Messi,atarejea uwanjani baada ya miezi 3.
Joyce Shedrack
July 21, 2024
Share :
Klabu ya Inter Miami ya Nchini Marekani anayoitumikia mchezaji Lionel Messi imempongeza mchezaji huyo wa Timu ya Taifa ya Argentina kwa kufikisha mataji 45 baada ya kutwaa ubingwa wa Copa America jumapili iliyopita.
Sherehe hiyo fupi imefanyika alfajiri ya leo katika uwanja wa Chase kabla ya mechi yao dhidi ya Chicago Fire ,Inter Miami wakimpa heshima nahodha wao kwa kuwa mchezaji mwenye mataji mengi zaidi katika historia ya soka Duniani akiwa ameshinda jumla ya mataji 45 kwenye mashindano yote rasmi ngazi ya klabu na timu ya Taifa yaliyochini ya UEFA.
Messi aliingia uwanjani akiwa anachechemea huku mguuni akiwa amevaa kiatu maalumu kwa watu wenye majeraha ya miguu ‘orthopedic shoe’ hii ni baada ya kuumia kwenye fainali ya Copa America dhidi ya Colombia na kupata jeraha la mguu ambalo litamuweka nje kwa miezi mitatu