pmbet

Inter watwaa ubingwa Serie A mbele ya AC Milan

Sisti Herman

April 23, 2024
Share :

Baada ya ushindi wa 2-1 jana dhidi ya watani zao AC Milan, klabu ya Inter Milan wametawazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu soka nchini Italia (Serie A) baada ya kufikisha alama 86 ambazo haziwezi kufikiwa kwenye michezo iliyobaki na washindani wao hao ambao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 69.

Kwenye mchezo huo ulichezwa kwenye dimba la San Siro, mabao ya Inter yamefungwa na Francesco Acerbi na Marcus Thuram huku goli la pekee la AC Milan likifungwa na Fikayo Tomori.

Hilo linakuwa taji la 20 la Serie A kwenye historia ya klabu hiyo sawa na AC Milan.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet