pmbet

Internet yasababisha kufungwa kwa Ubalozi wa Marekani Tanzania

Eric Buyanza

May 14, 2024
Share :

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umefungwa kwa siku mbili kutokana na ukosefu wa mtandao wa 'internet' iliyoathiri nchi kadhaa za Afrika Mashariki.
 

"Kwa sababu ya huduma duni za mtandao kote nchini, ubalozi hautafunguliwa kwa umma," ubalozi ulisema kwenye chapisho kwenye X (zamani Twitter) siku ya (jana) Jumatatu.
 

Ubalozi huo umeahirisha miadi yote ya konsula kwa siku ya Jumanne na Jumatano hadi mambo yatakapotengamaa.
 

Ubalozi huo, hata hivyo, utaendelea kupatikana kwa makusanyo ya visa na kushughulikia kesi za dharura zinazohusisha raia wa Marekani.
 

Mtandao wa internet ulipotea tangu Jumapili asubuhi, umesababisha umeathiri huduma za intaneti nchini Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda.
 

Hitilafu hiyo imetokana na kukatika kwa nyaya za chini ya bahari zinazounganisha eneo hilo na dunia nzima kupitia Afrika Kusini, mtaalam wa sekta hiyo Ben Roberts aliambia BBC.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet