Iran isitumie Hormuz kuzitisha nchi za Ghuba - Qatar
Eric Buyanza
May 13, 2026
Share :

Qatar imesema Iran haipaswi kutumia Mlango Bahari wa Hormuz, iliyoufunga tangu kuanza kwa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri hiyo ya kiislamu Fenruari 28, kama njia ya kuyahadaa mataifa ya Ghuba.
Akizungumza na waandishi habari mjini Doha akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Uturuki Hakan Fidan, Waziri Mkuu wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, amesema Iran haitakiwi kutumia Mlango huo wa Bahari kama silaha ya vita, kuyatisha na kuyashinikiza mataifa ya Ghuba.
Qatar na Uturuki ni washirika wa karibuni, walioibuka kuwa wapatanishi katika vita vya Iran na Marekani, wakiwa pamoja na mwenzao Pakistan. Al Thani amesema hawaungi mkono vita vinavyoendelea na ni lazima waongeze juhudi za kumaliza mivitano inayoshuhudiwa katika eneo hilo la Mashariki ya Kati.
”Hatuungi mkono kurejea kwa vita. Tunapaswa kuelekeza nguvu zetu kuiunga mkono Pakistan ili kutatua suala hili na kusitisha vita haraka iwezekanavyo na kumaliza pia hali inayoonekana sasa katika kanda nzima."
Mataifa ya Guba yameathirika na vita hivyo baada ya Iran kurusha makombora katika mataifa hayo ikilenga kambi za kijeshi za Marekani na pia miundombinu ya raia, viwanja vya ndege, na maeneo ya nishati. Kufungwa kwa Mlango bahari wa Homruz kunakopitia asilimia 20 ya mafuta na gesi ya dunia pia kumesitisha meli muhimu za biashara za mataifa hayo ya Guba, hali inayoendelea kuathiri chumi zao.





