pmbet

Iran kumnyonga mtu anayetajwa kufanya ujasusi kwa ajili ya Israel

Eric Buyanza

September 17, 2025
Share :

Iran imemhukumu kunyongwa mtu aliyetuhumiwa kufanya ujasusi kwa ajili ya Israel, kulingana na ripoti kutoka kwa vyombo vya habari vya serikali siku ya Jumatano mtu huyo alitambuliwa kama Babak Shahbazi.

Iran imetoa hukumu ya kifo kwa watu wengi inaowatuhumu kuwa na uhusiano na idara ya kijasusi ya Israel ya Mossad na kuwezesha shughuli zake nchini humo.

Visa vya hukumu ya kunyongwa kwa Wairani waliopatikana na hatia ya kufanya ujasusi kwa ajili ya Israel vimeongezeka kwa kiasi kikubwa mwaka huu, huku takriban hukumu tisa za vifo zikitekelezwa katika miezi ya hivi karibuni.

Vyombo vya habari vya serikali vilisema Shahbazi alifanya kazi na Esmaeil Fekri, mfungwa mwingine aliyenyongwa mwezi Juni kwa kufanya ujasusi wa Israel tangu mapema 2022.

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet