pmbet

Iran ni nchi ya kikatili inayopambana na ustaarabu - Netanyahu

Eric Buyanza

July 25, 2024
Share :

Netanyahu amewaambia wabunge wa Marekani kuwa "Maadui zetu ni maadui zenu" katika hotuba aliyoitoa kwenye bunge la Congress iliyokuwa na nia ya kutafuta uungwaji mkono katika vita vinavyoendelea ukanda wa Gaza. 

DW imeripoti kuwa kiongozi huyo alishangiliwa na wanasiasa wengi kutoka chama cha Republican wakati akitoa hotuba yake katika bunge hilo.

Netanyahu ametumia hotuba hiyo kuwashtumu waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina akisema wanapokea ufadhili wa siri kutoka kwa Iran.

"Tunapopigana na Iran, tunapambana na adui muuaji zaidi wa Marekani. Vita vyetu ni vita vyenu, na ushindi wetu utakuwa ushindi wenu." alisema Netanyahu kwenye hotuba yake.

Hata hivyo, mgawanyiko wa kisiasa kuhusu vita vya Gaza ulijitokeza wazi wazi baada ya wabunge kadhaa wa chama cha Democratic kutohudhuria kwa makusudi hotuba ya Netanyahu huku maelfu ya waandamanaji wanaopinga vita vya Gaza wakionekana nje ya bunge.

Akiizungumzia Iran, Netanyahu amedai nchi hiyo ni mhimili wa ugaidi unaoitishia Marekani, Israel na kwa ujumla ulimwengu wa kiarabu. Amekwenda mbali zaidi na kuielezea Iran kama nchi ya kikatili inayopambana na ustaarabu. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet