pmbet

Iran waacha barua Los Angeles baada ya kumaliza mechi zao.

Joyce Shedrack

June 22, 2026
Share :

Timu ya taifa ya Iran iliacha ujumbe katika chumba chao cha kubadilishia nguo kwenye uwanja wa SoFi Stadium siku ya Jumapili, ikiishukuru Los Angeles kwa ukarimu wake wakati wa Kombe la Dunia na kusema kuwa wanaondoka kwa heshima baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Belgium iliyowafanya kuwafanya waendelee kuwa na matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano.

We leave with dignity': Iran players write heartfelt note in SoFi dressing  room after World Cup draw with Belgium | The Independent

Los Angeles imekuwa mwenyeji wa mechi zote mbili za Iran katika Kundi G hadi sasa, huku timu ikirejea katika kambi yao iliyopo Tijuana kati ya mechi hizo.

 

Iran imekuwa ikishiriki mashindano haya ikiwa imeweka makazi yake Tijuana na kusafiri kwenda Marekani kwa ajili ya mechi zake kutokana na vikwazo vinavyohusiana na uwepo wao nchini humo, huku baadhi ya maafisa na wafanyakazi wa timu hiyo wakizuiwa kuingia.

 

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa mipango ya usafiri wa kikosi hicho itaendelea kutathminiwa, huku mazungumzo ya kupunguza baadhi ya vikwazo hivyo yakiendelea.

 

"Kutoka Uajemi wa kale wa maelfu ya miaka iliyopita hadi Iran ya kisasa ya leo, roho ya Iran imeendelea kuwa hai na imara," 

 

"Asante Los Angeles kwa ukarimu wako.

 

"Tulikuja Los Angeles kwa fahari, tukashindana kwa heshima, na tunaondoka kwa utu na heshima."Imesema barua hiyo iliyoandikwa kwa mikono na Shirikisho la soka la Iran.

 

Iran walitoka sare ya 2-2 dhidi ya New Zealand katika mechi yao ya kwanza kwenye SoFi Stadium na watacheza mechi yao ya mwisho ya makundi dhidi ya Misri mjini Seattle.

 

 

 

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet