pmbet

Iran yaanika ngome yake ya siri ya makombora chini ya ardhi

Eric Buyanza

November 17, 2026
Share :

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limefichua kituo kikubwa cha chini ya ardhi kinachotumika kuhifadhi makombora, hatua inayolenga kuonyesha nguvu zake za kijeshi kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya miundombinu yake.

 

Katika video iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali, makamanda wakuu wa kijeshi wa Iran, akiwemo Mkuu wa Majeshi Ali Abdollahi na Kamanda wa Kikosi cha Anga cha IRGC Majid Mousavi, walionekana wakikagua mahandaki marefu yaliyojaa makombora ya balistiki, makombora ya masafa marefu, pamoja na magari maalumu ya kuyarushia.

 

Serikali ya Iran haikutaja eneo halisi lilipo kituo hicho, ukubwa wake, wala tarehe kamili kilipokamilika. Aidha, uchambuzi wa picha za video hiyo umebaini kuwa baadhi ya mahandaki yamepigwa picha kutoka pembe tofauti, hatua inayozua maswali iwapo sehemu za vituo vya zamani zimejumuishwa katika maonyesho hayo.

 

Msemaji wa IRGC alieleza kuwa Iran imelazimika kuhamishia mitambo yake mingi ya kutengeneza makombora na ndege zisizo na rubani (drones) chini ya ardhi. Alisema mkakati huo unahakikisha kuwa uzalishaji wa silaha hauathiriwi hata pale kunapotokea mashambulizi makali ya anga.

 

Wachambuzi wa siasa za Mashariki ya Kati wanasema kufichuliwa kwa kituo hicho ni ujumbe wa moja kwa moja wa kiusalama kwa Marekani na Israel.

Kwa miaka mingi, Iran imekuwa ikijenga mtandao wa mahandaki chini ya milima inayofahamika kama "miji ya makombora" ili kulinda silaha zake dhidi ya ujasusi na mashambulizi ya anga kutoka kwa maadui zake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet