Iran yaishambulia Israel kwa 'Drones' huku 99% zikilipuliwa
Sisti Herman
April 14, 2024
Share :
Jesi la Iran usiku wa Ijumaa imerusha makombora na ndege zisizo na rubani kuilenga Israel katika shambulio la kwanza la moja kwa moja kulipiza kisasi.
Shambulio hilo limesababisha uharibifu katika kambi moja ya jeshi la Israel. Milipuko ilisikika katika maeneo mbalimbali ikiwemo Tel Aviv na Jerusalem Magharibi wakati mifumo ya kutungua makombora ikikabiliana nayo.
Msemaji wa jeshi la Israel, Daniel Hagari, amesema shambulio hilo lilihusika ndege zisizo na rubani takribani 200 na makombora kadhaa, ingawa idadi kubwa yalitunguliwa kwa msaada wa Marekani na Uingereza.