pmbet

Iran yawaua wapelelezi wa Marekani na Israel

Sisti Herman

November 9, 2026
Share :

 

Iran imetekeleza hukumu ya mauaji kwa watu watatu. BBC News ikinukuu taarifa iliyotolewa na Shirika la habari la Mizan, linalohusishwa na idara ya mahakama nchini Iran, limethibitisha kuwa Hassan Deoband, Hamid Kazemi na Reza Zanganeh waliuawa kwa kutekelezwa hukumu hiyo Jumapili asubuhi.

Kwa mujibu wa shirika hilo, watatu hao walihukumiwa kifo pamoja na kunyang'anywa mali zao baada ya kupatikana na hatia ya kushirikiana kiutendaji na Israel na Marekani.

Mizan imesema hukumu hizo zilitekelezwa baada ya kuidhinishwa na Mahakama Kuu ya Iran.
Shirika hilo limeongeza kuwa watu wengine 10 walikamatwa kuhusiana na kesi hiyo, huku washtakiwa wengine wakihukumiwa vifungo vya kati ya miaka mitano na 10 jela.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet