pmbet

Iran yawazika viongozi wa kijeshi waliouawa na Israel

Eric Buyanza

June 28, 2025
Share :

Majeneza yakiwa kwenye bendera ya Iran, yenye picha za makamanda waliofariki yamezungukwa na umati mkubwa wa watu.

Mazishi ya kitaifa yanafanyika nchini Iran kwa takriban watu 60, wakiwemo makamanda wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia, waliouawa wakati wa vita ya siku 12 na Israel.
Majeneza yaliyokuwa yamefunikwa kwenye bendera ya Iran, yakiwa na picha za makamanda waliofariki yalikuwa yamezungukwa na umati mkubwa wa watu karibu na Enghelab Square katikati mwa Tehran.

Miongoni mwa wanaozikwa ni Mohammad Bagheri, afisa wa ngazi ya juu zaidi wa kijeshi nchini Iran ambaye alikuwa mkuu wa majeshi ya Iran.

Umati mkubwa wa waombolezaji waliovalia mavazi meusi wakiimba nara, wakipeperusha bendera za Iran na kushikilia picha za waliouawa.

Mazishi hayo pia yatajumuisha pia Hossein Salami, kamanda mkuu wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, pamoja na wanasayansi kadhaa wa nyuklia kama vile Mohammad Mehdi Tehranchi, ambaye alikuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Azad mjini Tehran.

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet