Iraola atuma ujumbe kwa viongozi wa Liverpool
Eric Buyanza
July 22, 2026
Share :

Kocha wa Liverpool, Andoni Iraola, ameonyesha wasiwasi kuhusu maeneo mawili muhimu ndani ya kikosi chake na kutoa wito usio wa moja kwa moja kwa viongozi wanaohusika na usajili kuongeza kasi ya kuimarisha timu katika dirisha hili la majira ya kiangazi.
Hadi sasa, Liverpool imemsajili mchezaji mmoja pekee, Victor Munoz, mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na Hispania, kutoka Osasuna.
Pia, Iraola amesisitiza kuwa hataki kuona nyota wake Alisson Becker na Alexis Mac Allister, ambao wanawindwa na klabu za nje ya England, wakiondoka, akieleza kuwa badala yake anahitaji kuongeza wachezaji wapya ili kuimarisha kikosi.
Je, unadhani Liverpool wanahitaji usajili zaidi kabla ya msimu mpya kuanza?





