pmbet

Ishu ya Florent Ibenge na klabu ya Simba iko hivii

Eric Buyanza

May 8, 2024
Share :

Klabu ya Simba iko katika nafasi nzuri ya kumtwaa kocha Florent Ibenge, baada ya mwenyewe kuomba kuondoka ndani ya timu ya Al Hilal ya Sudan, huku uongozi wa timu hiyo ukiendelea kupambana kumbakisha. 

Wakati hayo yakiendelea, Klabu ya Simba iko mbioni kuwasajili wachezaji wawili wa timu ya Hafia FC ya Guinea, Mohamed Damaro Camara mwenye miaka 21, na Ousmane Fernandez 'Drame', 23.

Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo tofauti vya habari za michezo Afrika, zinaeleza kuwa kocha huyo amekaa vikao viwili na mabosi wa Al Hilal wakimweleza kuwa wana imani naye, lakini mwenyewe amesisitiza kuwa anataka kuondoka na sababu kubwa ni kutaka kuifundisha timu inayocheza Ligi Kuu na kupambania mataji.
"Kwenye majadiliano ya hatima yake, viongozi wamemweleza kocha kuwa bado wana imani na utendaji wa kazi yake na wanataka kuendelea naye, lakini ameng'ang'ania kuondoka kwa sababu timu kwa sasa haichezi ligi kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Sudan," vilisema vyanzo hivyo.

Licha ya kwamba Al Hilal huenda ikacheza Ligi Kuu Tanzania Bara nchini, baada ya maombi yao kukubaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), lakini kocha huyo bado anaonekana hajaridhika na hilo.

Ibenge anatajwa kuwa kwenye orodha ya wanaotakiwa na Klabu ya Simba na kupewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mkuu, baada ya kuondoka, Abdelhak Benchikha, huku kitendo cha kuomba kuondoka Al Hilal kikionekana kuwa huenda tayari ameshafikia makubaliano na klabu hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet